Kulingana na shirika la habari la Abna likinukuu shirika la habari la Palestina Shahab, Mahakama ya Kimataifa ya Haki inatarajiwa kutoa uamuzi wake leo Jumatano kuhusu hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuweka mzingiro huko Gaza na kuzuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, jambo ambalo linahesabiwa kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Uamuzi wa mahakama - huenda - ukawa ushauri wa kisheria na usio wa lazima, lakini jambo hili linaweza kuongeza shinikizo la kimataifa kwa utawala wa Kizayuni ili ushirikiane na Umoja wa Mataifa na kutoa idhini ya kuingia kwa misaada zaidi ya kibinadamu huko Gaza.
Ikiwa uamuzi huu utatolewa, utakuwa uamuzi wa tatu wa Mahakama ya Hague kuhusu vitendo vya utawala wa Kizayuni tangu kuanza kwa vita huko Gaza.
Your Comment